Mwanasiasa Julius Malema Kuanzisha Maandamano ya kum'ngoa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma

Mwanasiasa Julius Malema na Chama chake EFF wamepanga kuanzisha maandamano ya kum'ngoa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma leo.
Maandamano yasio na kikomo yataanzia Church Square katikati ya jiji la Pretoria. Julius Malema akiwa anawahutubia wafuasi wake mbele ya Mahakama Kuu Pretoria aliwaambia kuwa maandamano yatamaliza pindi watakapojisikia kuondoka, lakini hawatakuwa na nia hiyo ya kuondoka.
Na pia amewahataadharisha Polisi kutoingilia maandamano yao, amewaambia kazi yao ni kuhakikisha wanapatiwa usalama na si vinginevyo.
Amesema hana haja ya kuomba kibali cha maandamano kutoka Polisi au Mahakamani kwani ni haki yake kisheria. Amewaambia Polisi yeye kama Julius Malema Kazi yake nikuandaa Maandamano na ana hakikisha yanafanyika na Polisi kazi yao ni kuwalinda.
Maandamano yanaanza rasmi leo tarehe 2016 November 02 kuanzia saa 12 za asubuhi mpaka hapo Zuma atakapo achia nchi. Amesema uhuru wa Afrika Kusini haukupatikana kirasihi halafu yeye Zuma aje waibie rasilimali zao, wakati watu wengi waliuwawa kupigania uhuru.