Ommy Dimpoz amesema kuwa hana bifu na Diamond, na amesema kuwa hawajagombana kwa sababu ya Wema Sepetu. Hii inakuja baada ya Diamond kuachana na tetesi kuwa baada ya Diamond kuachana na Wema, kwamba Ommy Dimpoz alikuwa anatoka na Wema. Ila jana katika kipindi cha Playlist cha Times Fm Ommy Dimpoz kakataa kutoka na Wema na hana bifu na Diamond.
|
Ommy Dimpoz, Wema na Diamond |
Alichojibu Ommy Dimpoz kuhusu Bifu lake na Diamond 'Mimi na Diamond hatujagombana kwa sababu ya Wemasepetu, kuna upepo tu Mbaya umepita naamini mambo yatakuwa sawa muda si mrefu yatakwisha tu, ila napenda hizi TEAM ziendelee kuwepo zinaongeza ushindani' alisema @ommydimpoz Leo kwenye #ThePlaylist ya 100.5 Fm na @lilommy