Serikali yaainisha namna ya kukifanya kinywaji cha Gongo kuwa salama kwa matumizi

Akizungumza Jumanne hii bungeni mjini Dodoma, Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage, wakati akijibu swali lililoulizwa na mbunge Gimbi Dotto Masaba, mbunge wa viti maalumu lililohoji, Ifikapo mwaka 2025 Tanzania inafikia uchumi wa kati,Je? “serikali inampango gani wa kunzisha na kuhalalisha viwanda vya kutengeneza pombe aina ya Gongo ili kuchochea uchumi wa nchi?”

“Muheshimiwa spika viwanda anavyosema muheshimiwa Gimbi Dotto ni tabaka la viwanda vidogo sana na viwanda hivi ni fursa ya sekta binafsi kuwekeza,serikali inalenga viwanda vikubwa sana na miradi ya kimkakati kuhusu kuhalalisha pombe aina ya Gombo kama ilivyo sasa ni jambo ambalo haliwezekani ila sekta binafsi inashauriwa kuanzisha viwanda vitakavyo tumia malighafi itakayo tengeneza kinywaji hicho kwa lengo litakalo zalisha viwango vya usalama na ubora wa chakula,”amesema Mwijage.
“Naomba nirudie kinywaji hicho kwa kizingatia ubora na usalama wa mnywaji, moja ya kigezo muhimu kuanzisha kiwanda ni uwepo wa soko kutokana na wananchi kupendelea kinywaji hichi cha Gongo kuwashauri wadau wa sekta hii kuwasiliana na sekta za Sido ambazo zinapatikana mikoa yote ili kupata muongozo juu ya uanzishaji wa viwanda bora na salama wa aina hii upande wa makampuni makubwa ya pombe nawashauri wachangamkie fursa hii kwa kutengeneza pombe yenye ladha ya Gongo hii kwani baadhi ya wateja ni ile radha inayowavutia na kupendelea kinywaji hicho,”amesisitiza.
“Faida za kinywaji cha Gongo zinafahamika, wataalamu wangu wana uwezo wa kujua faida ya kinywaji hiki tatizo letu ni usalama, kwahiyo mimi nitawaelekeza wataalam wangu muheshimiwa mbunge waje kwenye jimbo lako kusudi wahakikishe kwamba kile kinywaji kitengenezwe salama,lakini kwenye jimbo langu nilikwambia watu wengi wanaokunywa gongo hawapendi gongo ila wanapenda ladha yake, sasa tutatafuta ladha tuwatengenezee kinywaji salama chenye ladha ya gongo.”
Bongo 5