TUKIO: Fiesta 2016 Ilifungwa rasmi na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo , Mh Nape Mosses Nnauye

Mh Nape Mosses Nnauye akiwa na Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa  Afrika ya Kusini Ndg. Nathi Mthehwa ( wanaonekana pamoja pichani ) walifunga rasmi Msimu huo hapo jana pale Escape One Mikocheni.

Picha linaanza hata Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo yuko sawa ; jana Mh Nape Nnauye alionyesha utumbuizaji uliotukuka wakati tukitoa #Shukrani na kuhitimisha msimu wa #Fiesta2016.



Balozi wa Afrika ya Kusini hapa Tanzania, Thamsanqa Dennis Mseleku alikuwa miongoni mwa wageni waliohudhuria tukio la jana pale Escape One. Baada ya Mh Nape Nnauye kucharaza nyuzi za gitaa Wasauzi wakasema "haaaataa, lazima tulipe" . Hapo ndipo Balozi Thamsanqa Mseleku alipokamata gitaa na kuimba muziki #Mubashara.

 Mkurugenzi Mkuu wa #CloudsMediaGroup, Joseph kusaga akisalimiana na Waziri wa Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa  Afrika ya Kusini Ndg. Nathi Mthehwa. Wengine pichani ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo , Mh Nape Nnauye na anayeonekana mwishoni ( nyuma ) ni Balozi wa Afrika ya Kusini hapa Tanzania ,Thamsanqa Dennis Mseleku.

Mwenyekiti wa Kamati ya Fiesta Seba maganga alizungumza mengi lakini kubwa zaidi ni #Shukrani

Navy Kenzo ni miongoni mwa Wasanii waliofika Escape One jana. Mbele ya Mh Nape, walitoa #Shukrani kwa Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa  Afrika ya Kusini Ndg. Nathi Mthehwa kutokana na mapokezi mazuri wanayopata wanapokwenda huko kwa Madiba kwa ajili ya shughuli za kisanaa hususan kutengeneza Video.
Je, unaamini ipo siku Wanamuziki wa South watakuja Tanzania kufanya video na 'madirector' wa Tanzania? 

Chanzo: Clouds