Wabunge wa YANGA wameamua kuungana na kuunda tawi la Yanga Bungeni

WABUNGE wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambao ni mashabiki wa Yanga wameamua kuungana na kuunda tawi la Yanga Bungeni. Kuelekea azimio hilo hapo jana bungeni Dodoma kulifanyika uchaguzi wa viongozi wa muda ambapo viongozi wafuatao walichaguliwa.

 A. VIONGOZI. ▪ Mwenyekiti - Venance Mwamoto. ▪ M/ Mwenyekiti - Ridhiwani Mrisho Kikwete.

▪Katibu Mkuu -Hafidh Ally Tahir( Amefariki usiku kuamkia leo) ▪Naibu Katibu - Hamidu Bobali

▪Mweka Hazina - Martha Mlata. ▪Msaidizi - Abdallah Ulega.

B. Wajumbe wa Kamati ya Utendaji. Grace Kihwelu. Halima Mdee. Seif Gulamali. Gibson Meiseyeki. Issa Mangungu. Dotto Biteko.

C. Baraza la Wadhamini Freeman Mbowe. Mwigulu Nchemba Hawa Ghasia.

Ili uwe mwanachama wa tawi hili ni lazima uwe Mbunge pia mwanachama wa Yanga, Mchakato unaendelea wa uundwaji kamili wa tawi hili bungeni.

Uongozi wa Naipenda YANGA unawapa pole wanachama wa Yanga Bungeni kwa kufiwa na katibu Mkuu wa tawi hilo ambaye amechaguliwa jana na kufariki usiku wa kuamkia leo pia tunawatakia kila la heri wabunge wanachama katika mchakato huu, ni mategemeo yetu tawi hili litakuwa na tija katika ustawi wa Yanga yetu.

 DAIMA MBELE NYUMA MWIKO. -

Chanzo: Naipenda YANGA