WAZIRI WA ARDHI: Ni Marufuku kwa Mtu aliyeukana Uraia wa Tanzania kumiliki Ardhi

Waziri wa Ardhi, amesema ni marufuku kwa mtu aliyeukana uraia wa Tanzania kumiliki ardhi kwakuwa ni kinyume cha sheria na akasisitiza kuwa umiliki wa ardhi ni kwa raia pekee.

Aidha, wakati akihutubia Waziri wa ardhi Willium Lukuvi amewataka wapima ardhi Tanzania kuhakikisha wanatimiza lengo la kupima na kutoa hati 400,000 ifikapo mwezi Juni mwaka 2017.

Akaongeza kuwa wananchi kutoa taarifa za raia wa kigeni wanaomiliki ardhi kinyume cha sheria na serikali itazitwaa ardhi hizo.