WALIOKOSA MIKOPO WACHANGIA SH900 MIL

Kuna usemi unasema 'Kufa kufaana' Ingawa wanafunzi 32,293 wamekosa mikopo ya kugharamia elimu yao katika vyuo mbalimbali nchini, wameisaidia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kukusanya fedha zinazotosha kuwalipia ada wenzao 646 kwa mwaka.

Kila mwanafunzi wakati wa kuomba mkopo HESLB hujaza fomu huku akiambatanisha na ada ya Sh30,000 ambazo hazirudishwi.

Kwa hesabu za kawaida, jumla ya fedha zilizochangwa na wanafunzi hao ni Sh968.7 milioni ambazo zinaweza kulipa ada ya mwaka mmoja wa masomo kwa wanafunzi 646 katika vyuo vikuu mbalimbali, bila kujumlisha gharama