ELIMU BIASHARA: KILIMO CHA MATIKI NA UPATIKANAJI WA SOKO

ELIMU BIASHARA Ukiwa Una Uhakika wa Kuvuna Tikiti ukubwa wa Saizi hii na kuendelea, huna haja ya Kuwaza Sokoni kutakuaje kwa maana Bei laazima itakua ni reasonable kuanzia 2,000/= kwa tikiti moja au zaidi, kwa sababu mtaani kama hilo wananunua kuanzia 4,000/= mpaka 8,000/=

. Hapa ndo Wakulima wa Hela wanawazaga apate matikiti kama hayo 5,000 tu kwa bei ya 2,000/= si atakua ana Milioni Kumi tayari. .. . Au akute soko zuri auze kwa 3,000/= si atakua na 15m. Basi mawazo hayo Yakimlevya keshokutwa anatafuta shamba anakodi, anaenda Kariakoo ananunua Mbegu anapanda, Baada ya siku 75 akishakata maji anashangaa matikiti yake yanafanana na yale ya 8,00/= sokoni na 1,500/= mtaani. Atakaa chini atapiga yowe kapata hasara, atawaambia waliomshauri waongo, atalalamika Kilimo akilipi na mengineyo. .

. Alafu anashangaa Jirani yake tu kavuna na tayari ameshaanza msingi wa Mabanda ya Kuku site kwake, ili hata kama next time asipovuna au akavuna akapata Hasara, atachota kidogo kwenye mradi wa kuku au kukopa arudi tena shambani kwakua anaamini kilimo ni kama biashara nyingine, hasara ni kawaida sana, tena huku uwezekano wa Kupata Hasara ni Mkubwa zaidi ya biashara za kawaida. Lazima uwe risk taker, na sio unawaza pesa.

Huku pesa zinakujaga zenyewe kama zitakavyoanza kuja January next year, na Hivi Mvua hamna watu hawajalima, anzeni kutunza vyakula na tuhamie kulima mazao ya Nafaka. Picha ya Tikiti kwa Hisani ya mkulima Renatus.

By Man Dea
Instagram :@elimu_biashara