CHELSEA WAJIKITA KILELENI KWA ALAMA SITA



Chelsea wameweka pengo la alama sita na kuendelea kubaki kileleni mwa ligi kuu soka England baada ya goli alilofunga kiungo Cesc Fabregas kipindi cha kwanza kuwa pekee na la ushindi.



Fabregas alipachika goli hilo kwa ufundi wa hali ya juu kwa kuupeleka mpira kwenye kona ya kushoto ya lango la Sunderland baada ya kupokea pande safi kutoka kwa Willian na kuwa ushindi wa kumi mfululizo kwa Chelsea

Ulikuwa ni ushindi muhimu sana kwa Chelsea baada ya Arsenal kuteleza siku ya Jumanne kwa kuchapwa 2-1 na Everton na hii inamaanisha vijana wa Antonio Conte watakuwa kileleni mwa ligi hiyo kwa msimu huu wa Christmas.
#BBC