MAMBO KUMI YALIYOTIKISA NCHI 2016

Dar es Salaam. Zikiwa zimebaki siku 27 kumaliza mwaka 2016, wachambuzi wa uchumi, siasa na jamii wamebainisha mambo makuu 10 yaliyotikisa nchi huku wakiitaka Serikali kuyafanyia kazi katika mwaka 2017.

MAMBO KUMI YALIYOTIKISA NCHI 2016


Tangu mwaka uanze, kumekuwa na matukio mbalimbali yatokanayo na majanga ya asili, uhalifu, ya kisiasa na mengine mengi ya utendaji wa kila siku wa Serikali.

Miongoni mwa mambo hayo ni tukio la tetemeko la ardhi lilioukumba Mkoa wa Kagera, ajali za barabarani, vita dhidi ya rushwa, mauaji ya kinyama yakiwamo ya askari polisi, mtikisiko wa uchumi, utumbuaji wa majipu, kesi za vigogo mbalimbali, bei kwa sukari na operesheni Ukuta.

Katika mjadala wake, Profesa wa elimu wa katika chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Kitila Mkumbo alisema pamoja na taifa kupitia katika matukio hayo makubwa yakiwamo yaliyosababisha kupoteza roho za Watanzania mwaka huu, kwake tukio kubwa ambalo limeacha historia katika Taifa ni kumpata Rais mpya, Serikali mpya na ajenda mpya.

Alisema mambo hayo mapya yamewawezesha Watanzania kuelewa ile dhana iliyokuwa ikipigiwa kelele miaka mingi kuwa madaraka ya Rais ni makubwa mno na yanapaswa kuangaliwa upya na kupunguzwa. “Uamuzi wa Rais kuamua kuzuia Watanzania kufanya siasa ina maana vyama vya siasa vipo kifungoni, na hii ina maana kuwa yale malalamiko yetu kuwa Rais ana madaraka makubwa yaliyoonekana kuwa ni nadharia, sasa ametusaidia kuona kuwa kulikuwa na hoja,” alisema Profesa Mkumbo.

Katika uamuzi huo, vyama vya siasa vilizuiwa kufanya mikutano ya hadhara na wakati fulani hata ya ndani, jambo lililozaa mpango wa Chadema wa kupinga ilichoita udikteta (Ukuta) uliotikisha nchi kutokana na mabishano baina ya chama hicho na Jeshi la Polisi. Hata hivyo, baadaye mpango huo ulisitishwa kwa maelezo kwamba ungekuja kwa sura nyingine na bila taarifa.

Profesa Kitila aliongeza kuwa kutokana na madaraka makubwa aliyonayo Rais kama taasisi, siku moja akitokea mtu asiye na busara huenda akaipeleka nchi katika hatari na tukapata matatizo makubwa kama taifa