SERIKALI YAKANUSHA TAARIFA ZA KUZUIA WATUMISHI WA UMMA KUTOKOPA KWENYE MABENKI

Serikali imekanusha taarifa zilizosambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii kuwa Watumishi wa Umma wamepigwa marufuku kukopa Benki, SACCOS, VICOBA na Taasisi mbalimbali za kifedha.



Serikali imesema taarifa inayosambazwa, ambayo imetafsiri mawasiliano ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni ya kupotosha, hivyo watumishi wote wa umma wanaombwa kuipuuza.

Vilevile watumishi wa umma wametakiwa kuzingatia kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali HAINA mamlaka ya kuzuia wala kuruhusu mtumishi yeyote wa Serikali kukopa au kutokopa katika Taasisi yoyote ya Fedha nchini.