MDOSI HAKUNIDUNDA INDIA- FRANCIS CHEKA

Bondia Mtanzania Francis Cheka ambaye mwishoni mwa wiki alipoteza pambano lake nchini India alilopigana na raia wa nchi hiyo Vijender Singh, ameibuka na kusema kuwa mpinzani wake huyo hakumpiga, ila alibebwa na mwamuzi.



Akizungumza kwa njia wa simu kutoka nchini India, Cheka amesema katika raundi hiyo ya tatu, alipata tatizo katika kifaa chake cha kulinda meno kwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na kikohozi, na wakati anakifanyia marekebisho, ndipo mwmuzi akatangaza mshindi, bila kumuuliza Cheka mwenyewe kama alikuwa anaendelea au la.

Pia Cheka amekanusha taarifa za kuwa amlipoteza pambano hilo kwa kuwa akili yake ilikuwa katika pambano lililoko mbele yake dhidi ya Dulla Mbabe.