BARACK OBAMA AMEWAHIMIZA WANA DEMOCRATIC KUPIGANIA OBAMA CARE

Barack Obama amewahimiza wanachama wa chama cha Democratic kupigania sheria yake ya bima ya afya ambayo utawala wa Donald Trump umeahidi utaibatilisha upesi baada ya kuingia madarakani. Kwenye mkutano wa faraghani wa saa mbili, Bw Obama aliwahimiza wabunge wa chama hicho kuitetea sheria hiyo, huku wanachama wa Republican nao wakichukua hatua kufuta sheria hiyo. Makamu wa rais mteule Mike Pence pia alikuwa katika bunge la Congress, ambapo alisema chama chake kitafuta sheria hiyo ambayo hufahamika sana kama Obamacare. Sheria hiyo iliwezesha takriban Wamarekani 20 milioni zaidi kupokea huduma ya afya.

#BBC