TANESCO YAIKATIA UMEME HOSPITALI, WAGONJWA WATAHARUKI

Wananchi wa Kilwa Kivinje na wilaya ya Kilwa wameingiwa na taharuki baada ya shirika la umeme wilaya ya Kilwa (TANESCO)kukata umeme katika hospitali ya wilaya hiyo maarufu kwa jina la Kinyonga kutokana na kutolipwa kwa deni huku Jenereta la dharura likiwa limeharibika.

Kwa mujibu wa kituo cha Channel Ten kufuatia uwepo wa Tatizo hilo na kusababisha wagonjwa kushindwa kupata vipimo na baadhi ya upasuaji , baadhi ya wananchi hao wameiomba Halmashauri na serikali kutatua tatizo hilo baada ya kukatiwa kwa kutolipia shs Milioni 23 zinazodaiwa.

Kamati ya usalama wilaya hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ,Chiristopher Ngubiagai ilifika hospitalin hapo baada ya kupokea taarifa kwa wananchi na kupata taarifa huku Kaimu Mganga Mfawidhi Mketo akikiri kuwepo kwa hali hiyo inayokwamisha huduma.

Baada ya agizo hilo Channel Ten ilimtafuta Mkurugenzi ndipo ilimpata Mwenyekiti wa Halmashauri huyo Abuu Mjaka , ambaye alikiri kupata taarifa , licha ya kuwepo katika ofisi za halmashauri kila mara Na kuahidi kutafuta namna ya kutatua.