Chuo kikongwe zaidi katika ulimwengu wa nchi zinazozungumza Kiingereza kimeongoza katika orodha ya Vyuo bora duniani.

Chuo kikongwe zaidi katika ulimwengu wa nchi zinazozungumza Kiingereza na kilichotoa viongozi mashuhuri nchini Uingereza cha Oxford, kimeongoza katika orodha ya Vyuo bora duniani.

Chuo hicho kimepiku chuo kilichokuwa kikiongoza orodha hiyo kwa miaka 5 iliyopita, cha California Institute of Technology, ambacho kimeshika nafasi ya pili.















Oxford, walikosoma mawaziri wakuu wanne kati ya sita waliopita wa nchi hiyo, kimepiku chuo cha Marekani baada ya bajeti yake ya utafiti kuongezeka kufikia paundi bilioni 1.4 ($1.83bn), wakati matokeo ya utafiti wake ukiongezeka, anasema Phil Baty, mhariri wa orodha hiyo.

Lakini Baty anasema kujitoa kwa Uingereza kutoka katika Jumuiya ya Ulaya “ni hatari kubwa kwa mafanikio yetu” kwa kufanya kuwa vigumu zaidi kuwavutia wanataaluma wa juu zaidi na kuwaweka katika miradi ya utafiti.