Rais John Pombe Magufuli ametengua uteuzi

Rais John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu tawala wa mkoa wa Kagera Bw.Amantius Msole na kumfuta kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Bukoba Bw.Steven Makonda baada ya kubaini kuwa wamefungua akaunti nyingine ya benki kwa kutumia jina linalofanana na Akaunti rasmi ya kuchangia maafa iitwayo "Kamati Maafa Kagera" kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Aidha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhasibu mkuu wa mkoa huo Bw.Simbaufoo Swai kutokana na kuhusika katika njama hizo.
SOURCE: Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu.!