CHRIS BROWN HAKUPASUA SIMU YA SHABIKI MOMBASA



Video ilimchukua Chris Brown anawasili mjini Mombasa, Kenya, haioneshi kama aliipasua simu ya shabiki, tofauti na ripoti za mwanzo zilizosambaa mtandaoni.  Hata hivyo tayari Wakenya wameanzisha hashtag #DeportChrisBrown wakitaka afukuzwe Kenya - kama ilivyokuwa kwa Koffie Olomide.

Awali, NTV ya Kenya waliandika: Popstar Chris Brown smashes a mobile phone belonging to a fan as she attempts to take a selfie with him in Mombasa.

Vanessa Mdee na Alikiba watamsindikiza mkali huyo jukwaani.