DONALD TRUMP MATATANI KWA KAULI YA KEJELI DHIDI YA WANAWAKE ALIYOITOA MWAKA 2005

Mgombea wa Urais wa Marekani, Donald Trump ameingia matatani kwa mara nyingine tena baada ya kusambaa kwa video ya mwaka 2005 ambayo anasikika akiongea maneno makali ya jinsi anavyowachezea wanawake.



Kufuatia kusambaa kwa video hiyo iliyozusha hasira kali kwa Wamarekani, Trump ameomba radhi.
Kwenye video hiyo Trump anasikika akisema kuwa unaweza kufanya chochote kwa wanawake na kama ni staa hawawezi kukataa.

Anasikika pia akisema jinsi alivyotaka kulala na mke wa mtu na jinsi anavyopenda kuwabusu wanawake warembo kila anapowaona.

Viongozi wa juu wa Republicans wamelaani maneno hayo. Mpinzaki wake, Hillary ameyaaita ya kushtusha. "We cannot allow this man to become president," aliandika kwenye Twitter.

Bongo5