DARASA HURU: USIJISIFU NA MSHAHARA WAKO, JISIFU ULIVYOWEKEZA.

Najua wengi wetu ni wa Ajiriwa, na huwa tunafurahi sana zile tarehe zetu za kupokea Mishahara zikikaribia. Ndio huwa tunafurahia kwa sababu tumeridhika kuishi maisha ya kusubiri PAYCHECK kila mwisho wa mwezi.



Tulioajiriwa kiukweli ni kuwa TUNACHOLIPWA na TUNACHOMZALISHIA MUAJIRI haviendani. Yaan, kazi unazozifanya ni kubwa sana tena zenye kumuingizia muajiri faida za kutosha lakini unachokipata kama Mshahara ni kidogo sana.

Kwa hiyo Option kubwa ambayo Wafanyakazi wengi wanayo ni kuamua KUONGEZA BIDII kwenye kazi zao, KUFANYA KAZI MASAA MENGI zaidi ya yale ambayo muajiri wetu katupangia ili tu ahakikishe anapata kuongezewa mshahara au kulipwa Overtime au kuhakikisha anapandishwa Cheo kazini akiamini mshahara utapanda.

Huku akisahau kuwa mshahara ukipanda, kodi itapanda (PAYE), matumizi yanaweza ongezeka, manyanyaso kazini yanaweza ongezeka, na bila kuwaza kuwa gharama za maisha zitapanda. Anawaza kuongeza mshahara huku hakuna chochote anachowekeza.

Na kiukweli wafanyakazi wengi mshahara ukifika unapita kama sio wake vile, unakuta kuweka akiba hawezi, kusema kuwekeza hata kwa kununua Hisa au Vipande hana pesa, hata kumiliki kiwanja ni changamoto, kufanya biashara mtaji hamna (Labda kwa wale wafanyakazi wanaokopa ndio wanaweza kuwekeza). Wafanyakazi wengi wana FEEL PROUD OF THEIR SALARIES RATHER THAN INVESTMENTS kwa kuwa hakuna wanachoweza kuwekeza kupitia mshahara kama mshahara, labda akope.

Unafurahia Mshahara unaousotea mwezi mzima kwa kumuingizia boss wako Billions of money, huku ukijisahau kujisevia na kujiwekezea na wewe uwe na vyako.

Unapokea Mshahara unaishia kwenye Mavazi, Bia, Partying, Kutoa michango ya harusi, na kuhakikisha unakula vizuri, miaka inakatika kazini huna ulichowekeza mwisho wa siku muda wa kustaafu ukifika unaanza kupata Stroke, presha kupanda, ndio unagundua kumbe ungeweza kuanza zako hata kufuga kuku wa kienyeji kumi ambao kama umenunua kuku kwa Elfu saba ingekugharimu Elfu 70 tu kununua hao kuku lakini masikini ya Mungu hata hujui jinsi ya kufuga kuku.

Usikubali Mshahara ukupumbaze akili, ukipata kidogo hakikisha unakikuza ili na wewe siku ya mwisho uje uitwe BOSS.

Mwandishi: NOEL.
Namba ya Simu: #0659289597
Instagram: @erinoebusinessconsultancy