ANAANDIKA: David Kafulila
UTEKELEZAJI WA BAJETI 2016/17
Nilikuwa nasoma ripoti ya mwezi kuhusu hali ya uchumi inayotolewa na Bank Kuu.
Kilichonistua katika eneo la utekelezaji wa bajeti, wakati mwezi Agost Serikali ilitaraji kutumia 230bn kutoka makusanyo yake ya ndani kwajili ya matumizi ya maendeleo badala yake ilitumia 67bn tu sawa na asilimia 29% ,Wakati serikali ilitaji kutumia 263bn kutoka vyanzo vya nje lakini ilitumia 62bn sawa na asilimia 23%.Hii ina maana kwamba jumla serikali ilitaji kutumia 493bn kutoka ndani na nje lakini ikatumia 130bn sawa na asilimia 26% .Huu ni mfano wa mwezi mmoja na hakika mwenendo ni huu kwa miaka mingi sasa. kwamba bajeti ya maendeleo Tanzania inatekelezwa chini ya asilimia 30% na kuifanya iitwe BAJETI HEWA.