ELIMU BIASHARA: TUNAKOPI MALENGO KUTIMIZA LENGO



Nilikua najaribu kutafuta stori za wagunduzi au wafanyabiashara waliofeli nijifunze kwanini walifeli. Nikakutana na stori nyingi zaidi za wagunduzi na wafanyabiashara ambao wamefanikiwa. Lakini wakati nasoma zote hizi nikagundua hata hawa waliofanikiwa waliwahi kufeli mara nyingi tu huko nyuma kabla ya kufanikiwa, so still nikapata kitu cha kujifunza kutoa kwao ambalo ndoo lilikua lengo langu.
.
Hii inasaidia sana pale unapojikuta umekwama kwenye idea yako au umepata hasara kwenye biashara yako, wewe sio wa kwanza kuna yaliyowakuta, cha kufanya badilisha idea au boresa mbinu za kufanikisha idea yako. Tukisoma story za idea zilizofanikiwa mara nyingi tunajikuta tukitaka kukopi njia zao za mafanikio na mwishowe tunakuja kufeli mpaka pale tutakapotafuta njia zetu za Mafanikio kupitia kujifunza njia zao za kufeli na kufanikiwa.

Ushawahi kujiuliza kama aliyegundua Kibatari alimuiga aliyetengeneza Mshumaa? Yule mtaalam wa Karabai? Na aliyegundua Chemli aliwaza nini? Well wote wanaweza wakawa walikua na idea zinazofanana katika ubunifu na uundaji tofauti, na inawezekana kabisa wote hawa zamani walikua Mamilionea, Lakini mwisho wa siku sasahivi hao wote wanaweza wakawa wamefulia kutokana na Kugundulika kwa Nishati ya Umeme na Nishati ya Jua, na kama hawakuinvest sehemu. JIKUNG'UTE, JIPANGE, ANza.

By Man Dea
INSTAGRAM @elimu_biashara