Mtandao wa Facebook umeanzisha mfumo mpya wa mtandao mpya uliopewa jina la ‘Work Place’ ambao utasaidia makampuni kurahisisha mawasiliano kwa njia ya ujumbe wa video ya moja kwa moja.
Mfumo huo mpya umebuniwa na mtandao huo kwa ajili ya kuleta ushindani kwa mifumo mingine ya mawasiliano iliyopo kama Email na mingine.
Mfumo wa mawasiliano wa ‘Worl Place’ utaingia kwenye masoko mengine sawa na ule wa mtandao wa Microsoft wa Yammer ambao makampuni yanaweza kutumia sawa na ule wa Slack ambao ni wa mawasiliano ya ujumbe.
Facebook imekuwa ikiufanyia majaribio mfumo huo mpya ambao awali ulipewa jina la ‘Facebook at Work’ kwa muda wa miaka miwili na mpaka sasa zaidi ya makampuni 1000 tayari yanautumia.