HALOTEL KUZINDUA HUDUMA MPYA YA HALOPESA.

Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel Tanzania, imeadhimisha mwaka mmoja tangu ilipoanza kutoa huduma zake hapa nchini. Kwa kipindi hicho cha mwaka mmoja, Halotel imeweza kufikia malengo yake kwa kiasi kikubwa ikiwamo kuongeza idadi ya watumiaji wa mtandao wake. Kwa mujibu wa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hadi kufikia Septemba mwaka huu 2016, Halotel ilikuwa na watumiaji wa mtandao huo wapatao milioni tatu na nusu (3,500,000).



Lakini pia, ripoti ya robo ya kwanza na ya pili ya mwaka huu ya TCRA inaonesha kuwa, Halotel imekua kwa kasi kwa upande wa ongezeko la wateja. Kutokana na hali hiyo, tunaelekeza nguvu zetu zote katika kuboresha miundombinu yetu. Kwa mfano, hadi sasa tumekwisha jenga zaidi ya kilometa 20,000 za mkongo wa mawasiliano na zaidi ya vituo 4,200 kwaajili ya kupokea mawasiliano. Tumepeleka mitambo maalumu ya kuboresha mawasiliano katika vijiji 3,000 ambavyo awali havikuwa vimeunganishwa.

Kama wawekezaji wengine wote, Halotel imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mkuu huyo bwana Le Van Dai, alitumia fursa hiyo kuzindua huduma mpya ya Halopesa, huku akiwataka watanzania kujiunga na huduma hiyo, akidai kuwa imeenea sehemu kubwa nchini na ni ya haraka. ambapo itakuwa inapatikana kwa code namba ya *158*88#.

Kwa kutumia Halopesa mteja anaweza kufanya malipo mbalimbali kama vile kutuma na kupokea fedha, kupokea au kutuma fedha kupitia benki na kulipia huduma nyingine kama Luku, Dawasco, na ving’amuzi vya televisheni  mfano. ZUKU, mifuko ya jamii wa GEPF, TCU na Polisi na kununua muda wa maongezi kwa mtandao wa Halotel.