Hans van Pluijm bado yupo yupo sana Yanga

Kama wapinzani wa timu ya Yanga walikuwa wanafurahia kujiuzulu kwa kocha mkuu wa timu hiyo Hans van der Pluijm – imekula kwenu.
Hivi karibuni kocha huyo aliandika barua ya kujiuzulu kuifundisha timu hiyo huku kukiwa na tetesi kuwa mikoba yake inaenda kuchukuliwa na kocha wa klabu ya Zesco ya Zambia, George Lwandamina.

Klabu ya Yanga imeyakataa maombi ya kujiuzulu kwa kocha huyo huku ikidaiwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba amefanikiwa kumshawishi kocha huyo kuendelea kuifundisha timu hiyo baada ya kufanya naye kikao cha siri.
“#Done,” ameandika waziri huyo kwenye picha aliyoiweka kwenye mtandao wa Instagram akiwa kwenye mazungumzo na Pluijm.
Yanga
Bongo5