By Malisa GJ,
Wakati Tanzania ikiadhimisha miaka 17 ya kifo cha baba wa taifa Mwalimu Nyerere, nchini Malawi media zote na social media zimepambwa na habari za kupotea kwa Rais wa nchi hiyo Peter Mutharika. Jabari hiyo pia imepewa uzito katika media za kimataifa katika nchi mbalimbali za Afrika.
Kituo cha Televisheni cha Citizen cha nchini Kenya kimeripoti kupotea kwa Rais Mutharika kwa muda wa wiki 3 sasa tangu aondoke mjini New York, Marekani kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Rais Mutharika hajarudi nchini kwake tangu alipoondoka September 15 kuelekea Marekani. Hali hiyo imepelekea raia wa nchi hiyo kuweka hashtags kwenye mitandao ya kijamii zikisema #BringBackMutharika haswa kwenye Tweetter, na Facebook.
Taarifa ambazo hazijadhibitishwa zinasema kwamba Rais Mutharika ni mgonjwa na alipotoka Marekani alienda nchini Uingereza kwa matibabu. Inadaiwa matibabu hayo ndiyo yamesababisha asiweze kurudi nchini kwake hadi sasa. Lakini Ikulu ya Malawi imekanusha taarifa hizo na kusema Rais Mutharika ni mzima wa afya na haumwi lolote.
Jumatatu ya tarehe 10 October, 2016 shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) lilinukuu taarifa ya Ikulu ya Malawi kuwa Rais huyo si mgonjwa na atarudi nchini humo jumapili. Pia gazeti la #NyasaTimes limeripoti kuwa Rais huyo ni mzima wa afya. Chapisho la gazeti hilo la juzi jumanne September 11, 2016 liliandika "Fit and well President Mutharika returns to Malawi on Sunday".
Kufuatia habari kuwa Mutharika si mgonjwa kumeibua mijadala mikubwa kwenye mitandao ya kijamii, na kusababisha watu kuhoji anafanya nini Ulaya kwa mwezi mzima ikiwa haumwi.? Je anafanya starehe?
Ikiwa Mutharika atakuwa anafanya starehe huko Ulaya atakuwa ameingia kwenye rekodi mpya baada ya ile iliyowekwa na aliyekuwa Rais wa Togo Marehemu Gnassingbé Eyadéma ambaye aliwahi kuitelekeza nchi yake kwa miezi mitatu akaenda kula "starehe" nchini Ufaransa, akiwa na mabinti kadhaa warembo kutoka nchini humo.
Rais Eyadema alifariki mwaka 2005 baada ya kutawala nchi hiyo kwa miaka 38, na baada ya kifo chake mwanae wa kwanza Faure Gnassingbé akarithi mikoba yake, na amekuwa Rais wa nchi hiyo hadi sasa.
Hoja ya vyombo vya habari kudai kuwa Rais Mutharika amepotea inatokana na ukweli kwamba hajulikani alipo hadi sasa. Ikulu ya Malawi imekanusha kwamba hayupo Uingereza kwa matibabu, lakini haitaki kusema yupo nchi gani na anafanya nini. #BringBackMutharika
Malisa GJ