Viazi vitamu vyawapa Tuzo Wanasayansi



Wanasayansi wanne wamepewa tuzo la chakula la mwaka 2016 kwa kuimarisha viazi tamu, hatua ambayo iliwafaidi mamilioni ya watu kiafya. Walishinda tuzo hiyo kwa mfano wa kipekee wa urutubishaji wa kibaiolojia ,swala lililopiga jeki Vitamin A katika zao hilo.

Tangu mwaka 1986,tuzo hilo la chakula linalenga kutambua juhudi za kuimarisha ubora na wingi wa chakula kilichopo. Watafiti hao watapata dola 250,000 katika sherehe itakayofanyika Iowa nchini Marekani siku ya Alhamisi. Watatu kati ya waliopewa tuzo hilo -maria Andare,Robert Mwanga na Jan Low kutoka kituo cha CGIAR International Potato wametambuliwa kwa kazi yao ya kuimarisha rutuba ya viazi tamu.