MALISA J: Kwanini wateule wa Rais wanafanya mambo hovyo kiasi hiki?





Kwa mujibu wa ITV silaha hii ni mali ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga Ndg.Emmanuel Barnabas Mkumbo, ambayo aliitumia kumtisha askari wa usalama barabarani mkoani Morogoro akijifanya ni usalama wa taifa.



Yani DED Mkumbo alikamatwa kwa kosa la overspeed. Askari aliyemkamata akataka kumuandikia faini, lakini Mkurugenzi huyo akadinda. Akajitambulisha kuwa yeye ni Afisa wa Usalama wa Taifa, hivyo Askari huyo amruhusu aende. Askari akamwambia hata kama ni Usalama wa taifa ni muhimu kufuata sheria za usalama barabarani.

DED akakasirika. Akaanza kutoa maneno ya "hovyo" kwa Askari huyo. Badae akamtolea bastola na kumtishia kumuua. Askari huyo akawasiliana na wenzake, wakaja kumkamata. Kufikishwa Polisi ndipo ikajukikana kwamba Mkumbo ni DED wa Wilaya ya Mkinga na sio Afisa Usalama wa Taifa kama ilivyodaiwa.

Polisi wakamshikilia jana akalala rumande na leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Morogoro akikabiliwa na Mashtaka Mawili. Moja la kutishia kuua na jingine la usalama barabarani, ambapo ana makosa matano yanayohusiana na usalama barabarani.

#MyTake:

Nimesikitika kuona kuna wateule wa Rais waliokosa maadili kiasi hiki. Usalama wa taifa umegeuzwa kichaka cha kufanyia maovu. Kila mtu akitaka kufanya ujinga wake anajivika kwanza kilemba cha usalama wa taifa kisha anatekeleza uhalifu wake. Mnamkumbuka yule M/kiti wa UVCCM Arusha nae alifanya hayahaya ya DED.

Sasa jiulize kama DED anaweza kutumia idara ya usalama wa taifa vibaya, watumishi wengine vp? Nadhani kuna haja ya kufanya reform kwenye idara ya usalama ili isiendelee kutumika vibaya. Kwanini wateule wa Rais wanafanya mambo hovyo kiasi hiki? Hivi hawa ni wale wateule ambao Rais alitumia miezi mitatu "kuwascan" kabla ya kuwateua? Nasikia kuna mwingine katishia vyombo vya ulinzi kisa na yeye ni mteule wa Rais.

Wateule wa Rais wanafanya mambo yanayopaswa kufanywa na "vikatuni". Wangapi mnakumbuka Visa vya baba Ubaya, katuni ya Bi Mkora, au Singombingo za Kaboka Mchizi? Huyu aliyempiga mkwara Trafic kwa Bastola halafu mwishowe kibao kikamgeukia yeye, amenikumbusha katuni ya "Mikwara ya kichaa Chadogi". Bado tuna safari ndefu sana.!

Malisa GJ