MILLARD AYO WA CLOUDS APEWA TUZO



Dar es Salaam. Taasisi ya Great Hope Foundation (GHF) leo imemtunukia tuzo ya kuwa mfano wa kuigwa Mtangazaji maarufu wa kituo cha Radio cha Clouds Fm Millard Ayo.

Mgeni katika tuzo hizo zilizokwenda kwa jina la ‘Onesha uwezo’ Mkurugenzi mkazi wa Trademark East Afrika John Ulanga alisema Mtangazaji huyo alipambana na kufanikiwa kuonesha uwezo wake ambao sasa umekuwa na mafanikio makubwa kwake na taifa kwa ujumla.

"Millard aliweza kufanya kazi ya utangazaji katika changamoto nyingi ikiwemo kukatishwa tamaa na wazazi wake, kufanya kazi bila malipo kwa muda mrefu lakini leo uwezo unadhihirika,"alisema Ulanga.