Mvumbuzi wa nepi za kutupwa afariki dunia akiwa na miaka 94



Valerie Hunter Gordon, mama wa watoo sita aliyevumbua nepi za kutumiwa na kutupwa ameaga dunia nyumbani kwake karibu na Inverness akiwa na umri wa miaka 94. Familia yake inasema alifariki October 16 huko Beauly.


Aliovumbua nepi ya kwanza ya kutupwa iitwayo "Paddi" baada ya kumzaa mwanawe wa tatu Nigel, mnamo 1947 na baada ya kuchoshwa na kufua nepi za vitambaa. Nepi hizo awali zilitengenezwa kwa nyloni, karatasi na pamba. Bi Hunter Gordon alitengeneza mamia ya nepi kwa kuzishona kwa cherehani jikoni kwake, na kuzisambaza kwa rafiki zake huku akizifanyia ukarabati mara kwa mara.

Mumewe, Meja Pat Hunter Gordon, alilazimika kumsaidia kutengeneza nepi hizo aliporudi kutoka vitani Borneo.
Nepi 'mbovu' Akizungumza na BBC mnamo 2015, Bi Hunter Gordon amesema laiona kazi kubwa kufua nepi na ndipo akaanza kutafuta atakazoweza kutumia na baadaye kuzitupa.


"Nilidhani zauzwa - lakini zilikuwa hazipatikani kokote," alisema. "Ilishangaza sana kwamba haizjawahi kutengenezwa. Nilidhani itakuwa rahisi kwahivyo wacha nizitengeneze. Lakini haikuwa rahisi, ilikuwa vigumu kiasi .
"Kila aliyeziona alisema, Valerie, tafadhali nitengeneze na mimi moja? Kwahivyo niliishia kutengeneza kama nepi 600.

"Niliishia kwenye cherehani cha mamangu, kutengeneza nepi hizi mbovu." Paddis zilitumika badala ya nepi za tauli ,ambazo ilikuwa ni lazima uzioshe baada ya matumizi. "Kila mtu alitaka kuacha kusha nepi. Sikuhizi ni kama wanataka kurudi kuzifua tena - kila la kheri kwao," alisema Bi Hunter Gordon mwaka jana.

BBC