Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva ameitaka serikali kubadili muundo wa tume hiyo



Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva ameitaka serikali kubadili muundo wa tume hiyo ili iwe na ofisi na watumishi katika kila halmashauri nchini na ofisi ya Zanzibar. “Pamoja na hayo, Serikali inatakiwa kubadili muundo wa NEC ili kuwa na ofisi na watumishi katika kila halmashauri nchini na ofisi ya Zanzibar, hiyo itafanya tume ifanye kazi zake kwa uhuru zaidi tofauti na sasa ambapo kazi hizo zimekuwa zikifanywa na wakurugenzi wa halmashauri,” amesema.

Amesema baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, tume iliamua kufanya tathmini kwa lengo la kupata mrejesho juu ya utekezaji wa Uchaguzi Mkuu kutoka kwa wadau na kudai kuwa ni mara ya kwanza kwa tume kufanya tathmini tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993. “Tathmini hii imefanyika ikiwa ni mojawapo ya zoezi linalokamilisha mzunguko wa uchaguzi na kuanza kwa mchakato wa uchaguzi mwingine,” amesema.