NIGERIA: Mke wa Rais wa Nigeria hatomuunga mkono Buhari katika uchaguzi ujao kama hatotimiza haya



Mke wa Rais, Aisha Buhari amemuonya mumewe kuwa hatomuunga mkono katika uchaguzi ujao kama hatafanya mabadiliko katika Serikali yake. Aisha Buhari amesema mumewe "hawafahamu" wengi wa maafisa wakuu aliowateua serikalini na akadokeza kwamba Serikali imetekwa. Amesema kuwa "watu wachache" ambao huamua ni nani watateuliwa.