Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Emmanuel Mkumbo. Bado sababu za utenguzi hazijatajwa.
Mkurugenzi huyu ambaye uteuzi wake umetenguliwa, jana alifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumtishia kumuua kwa bastola Askari wa Usalama Barabarani. Uteuzi wa Mkurugenzi mwingine wa Wilaya ya Mkinga kuziba nafasi hiyo utafanywa baadaye.