SAIKOLOJIA: Watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kubuni wana kawaida ya kudharau wengine

Watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kubuni wana kawaida ya kudharau wengine na hata kujidharau wenyewe. Hutokea kwamba, wanaweza kufikiri na kubuni mambo makubwa kwa urahisi, kwa hiyo hudhani kuwa mambo hayo ni ya kawaida. Kwa hiyo wengine wanaposhindwa kufikiri na kubuni kama wao, basi huwadharau. 



Lakini kwa sababu ya uwezo huo mkubwa wa kufikiri na kubuni, hufanya kujirekebisha wao wenyewe mara nyingi kila wanapofikiria upya na mwishoe wanaweza pia kujidharau. Hawa ni watu wanaojua kuwa wanajua kwa sehemu kubwa,  na wasioyajua hujua kuwa hawayajui. 

Vilevile watu wenye akili chache na uwezo mdogo wa kufikiri hushindwa kutambua hali zao na hudhani kwamba wana uwezo mkubwa. Nao pia wana kawaida ya kudharau wengine lakini hawana kawaida ya kujidharau. Hawa ni watu wasiojua kwa sehemu kubwa yale wanaoyajua, na wasioyajua hawajui kuwa hawayajui.Maelezi haya kitaalamu hujulikana kama Dunning-Kruger effect