NSSF: Mapato Daraja Kigamboni yafikia Bil. 3

Daraja la Nyerere la Dar es Salaam limeliingizia Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) zaidi ya shilingi billioni 3 tangu lizinduliwe, Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Professa Godius Kahyarara amesema.



Aidha, Mkurugenzi huyo alisema mapato hayo makubwa yanatokana na uamuzi wa shirika kuepuka kutumia kampuni binafsi katika miradi yake yote, baada ya kushindwa kufanya vizuri katika miradi mingine ilizozipatia.
Kutokana na uamuzi huo, makusanyo kwenye miradi ya NSSF sasa yameongezeka huku mradi wa daraja hilo ukiingiza zaidi ya Sh. bilioni tatu tangu uzinduliwe Aprili 19.

Prof. Kahyarara alifanya mazungumzo na Nipashe baada ya 'kigogo' huyo kutembelea daraja hilo mwishoni mwa wiki iliyopita. Ujenzi wa daraja hilo, ambao uligharimu dola za Kimarekani milioni 128, ulianza mwaka 2012 na kufanywa na kampuni ya China Railway 15 Group ikishirikiana na kampuni ya China Bridge Engineering Group. 

 #Nipashe