Upepo mkali umeezua vyumba sita vya madarasa katika Shule ya Msingi Byamutemba mkoani Kagera na kujeruhi wanafunzi sita.
Kutokana na tukio hilo lililoathiri pia nyumba za wakazi wa eneo hilo ambazo idadi yake haijafahamika, Serikali imeifunga kwa muda usiojulikana shule hiyo, ikisubiri kuijenga baada ya taratibu kukamilika.
Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Limbe Mourice amesema majeruhi hao wamelazwa katika Kituo cha Afya Bunazi.
Kwa siku za karibuni Mkoa wa Kagera umekumbwa na mabalaa likiwamo tetemeko la ardhi liliua watu 17 na kusababisha nyumba zaidi ya 3,000 kuanguka na hadi sasa nyingi hazijajengwa.
#mwananchi