Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ameikabidhi Ofisi Bodi mpya wa Soko la Feri iliyoteuliwa hivi karibuni, baada ya ile ya zamani kuondolewa. Akikabidhi ofisi hiyo katika Soko hilo lililopo Feri Jijini Dar es Salaam, Mjema amesema, anaamini Bodi hiyo itafanya mabadiliko makubwa ili kuliweka soko hilo kuwa la kimataifa.
Mjema ameitaka Bodi hiyo, kubuni vitu mbali mbali vya burudani katika soko hilo, ikiwa pamoja na kuweka soko hilo katika hali ya usafi, Aidha Mjema ameitaka Bodi hiyo kuweka uzio ili kudhibiti uhalifu, kuwapa vitambulisho maalumu wafanyabiashara pamoja na uvaaji wa sare maalumu zilizo safi.
Katika hatua nyingine Mjema ameitaka Bodi hiyo kuongeza vyoo ili kuzingatia hali ya usafi na kuepuka magonjwa ya milipuko kwani eneo hilo pia kuna biashara ya mama lishe ambao hutoa huduma ya kuuza chakula, kwani soko hilo lina vyoo 3 tu ambapo ameagiza uwepo wa vyoo zaidi ya 20, Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya ameipa bodi hiyo Miezi mitano kuhakikisha inafanya mabadiliko hayo,kwani ataenda tena kutembelea Mwezi Machi mwakani.
Kwa upande wake Massaba amesema kuwa, tayari Bodi yake imeweka mikakati mizuri ya kuliinua soko hilo hilo, ikiwa pamoja na kuweka miundo mbinu katika hali ya usafi, usalama wa wananachi na mali zao.