VURUGU kubwa zimeibuka baina ya mkuu wa mkuu wa mkoa Arusha Mringo Gambo na mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema

VURUGU kubwa zimeibuka baina ya mkuu wa mkuu wa mkoa Arusha Mringo Gambo na mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo ya buruka nje kidogo ya jiji la Arusha.



Vurugu hiyo zimeibuka baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho gambo kuvuruga ratiba iliyokuwa imepangwa na waandaaji wa hafla hiyo ambapo kwa mujibu wa ratiba iyo ilikuwa imepagwa kuwa hotuba ya mkuu wa mkoa ingetanguliwa na waandaji wa shughuli hiyo akiwemo waandaji wa hafla hiyo,wafadhili pamoja na mbunge Lema.

Kabla ya vurugu hizo mkuu wa Arusha alikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexzanda Mnyeti swala ambalo liliibua mzozo mkubwa kwa wananchi walikuwa wamefika kushuudia tukio hilo la uzinduzi wakiwemo wafadhili waliofadhili mradi ambao ni shirika la kuhudumia afya ya mama na mtoto (maternity Afrika ). Baada ya kuanza kuhutubia mkuu huyo wa mkoa akielezea historia ya mradi huo ikiwe upatikanaji wa eneo la kujenga mradi wa hospitali hiyo gafla mbunge lema alipo simama na kupinga hotuba hiyo hiyo na kudai imejaa upotoshwaji na siasa ndani kwani yeye ndie aliyetafuta eneo hilo la ujenzi wa hospitali hiyo kutoka katoka kampuni ya mawala Advocate na sio kweli eneo hilo limetokana na maono aliyokuwa nayo Marehemu Advocate Nyaga Mawala ya mda mrefu. 

Chanzo @issamichuz