Wakurugenzi 3 wa Bandari wafikishwa mahakamani kwa kesi ya rushwa ya Bil 9



Vigogo watatu wa zamani wa mamlaka ya bandari akiwemo aliyekuwa mkurugenzi mkuu Ephraim Mgawe na mfanyabiashara mmoja, jana wamefikishwa mahakamani wakishtakiwa kwa makosa mawili ya kutoa na kupikea rushwa ya billioni 9.

Aidha, washtakiwa hao wanadaiwa kuomba na kutoa rushwa kutoka kampuni ya Leighton Offshore Pte. Ltd ili kuiwezesha kushinda zabuni ya kubadilisha boya kwenye ufukwe wa Mjimwema wa TPA jijini Dar es Salaam.
Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba jana.

Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Emmanuel Jacob, aliwataja washtakiwa wengine kuwa ni Mkurugenzi wa Uhandisi wa zamani wa TPA, Bakari Kilo (59), Meneja Manunuzi wa zamani wa TPA, Theophil Kamaro na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya DB Shapriya and Company Ltd, Kishor Shapriya.

#Nipashe