Sababu za Kampuni ya tajiri Dangote kupunguza kazi wataalamu 48



Kufuatia Mdororo wa Uchumi unaoendelea nchini humo, Kampuni ya tajiri Dangote imepunguza kazi wataalamu 48. Yasema kuwa haina fedha za kuwalipa. Ripoti zinasema kuwa hatua hiyo inatokana na gharama za kufanya biashara kupanda katika taifa hilo na kampuni hiyo imeshindwa kupata fedha za kigeni kuwalipa baadhi ya wataalamu wake wa kigeni.

Kampuni ya Dangote Group ni miongoni mwa kampuni zilizo na wafanyakazi wengi. Miezi miwili iliyopita, mtandao wa Bloomberg uliripoti kwamba bwana Dangote alipoteza dola bilioni 5.4 mwaka huu kutokana na kuanguka kwa thamani ya sarafu ya Nigeria, Naira.