Klabu ya Yanga leo imemteua bwana Jerome Dufourg kuwa CEO wa klabu hiyo



"Klabu ya Yanga leo imemteua bwana Jerome Dufourg kuwa CEO wa klabu hiyo. Jerome, ambaye amewahi kutumikia shirikisho la soka la Rwanda na klabu ya FC Talanta ya daraja la kwanza Kenya, amepewa majukumu ya kuendesha shughuli za klabu hiyo pamoja na mipango ya fedha ya Klabu hiyo ambayo mwaka jana kwa mujibu wa Yusuph Manji klabu hiyo iliingiza hasara ya zaidi ya billioni 1.5 ya kitanzania.

Jerome Dufourg, raia wa Ufaransa anategemewa kuwasili Tanzania siku za hivi karibuni na kuanza rasmi kibarua chake cha kuifanya Yanga kuwa bora Afrika mnamo November 19, 2016.