WEMA AKAMATWA NA POLISI CHINA AKIHISIWA NA MADAWA YA KULEVYA

Mkali wa Bongo movie Wema Sepetu wiki liyopita aliwekwa chini ya ulinzi kwa saa kadhaa huko chini baada ya kufananishwa na mwanamke raia wa Ghana anayetuhumiwa na kufanya biashara ya dawa za kulevya nchini humo.



Habari zinasema msichana huyo rai wa Ghana anatambulika kwa jina la Zahara kwa mujibu wa habari hizo Wema alikumbwa na mkasa huo katika Jiji la kibiashara la Ghouzhou, akiwa anafanya ‘shooping’ ya vitu mbalimbali,
Chanzo cha habari hii kinasema wema alitiwa nguvuni na Polisi waliokuwa wakimfatilia kwa muda mrefu akiwa katika jiji hilo.

Mmoja wa marafki wa Wema Sabiha Nassoro ambaye yupo nae huko China alithibitisha kutokea kwa mkasa huo huko China.

“Tukiwa katika pilikapilika za manunuzi ya vitu ghafla askari wa kike na wakiume walimuomba Wema kwenda kumhoji maswali na kisha wakamwachia lakini baada ya kama dakika 10 walimfuata tena na kumchukua hadi kituo cha polisi ambako walimhoji” alisema Sabiha

Sabiha aliongezea kuwa “tulipofika polisi walituonesha picha za Wema akiwa anazunguka mjini hapa tangu alipofika, inaonekana walikuwa wanamfatilia sana tangu alipo kuja”