ANZA LEO KUTIMIZA NDOTO ZAKO

ANZA LEO KUTIMIZA NDOTO ZAKO: Hauhitaji hadi ufikie Umri fulani ndio utimize #Ndoto zako. Haijalishi una miaka 19 au 20 bado unayo fursa ya kuanza sasa kutimiza ndoto ulizonazo, hakuna mtu atakaekuzuia usitimize ndoto zako kisa wanasema bado mdogo.

Haijalishi una miaka 35 au 40 bado unayo nafasi kubwa ya kutimiza ndoto zako, umri haukuzuii wewe kutimiza ndoto ulizonazo. Haijalishi wewe ni mstaafu basi ndio ukate tamaa ya kutimiza ndoto zako. Kumbuka Mmiliki wa Mgahawa maarufu leo hii wa KFC aliweza anza itimiza ndoto yake ya kupika KUKU akiwa na Umri wa miaka 65, hivyo hata wewe bado unayo nafasi hiyo ya kutimiza ndoto zako.

Haijalishi wewe kisa ni mama wa nyumbani basi uamue kuziua ndoto zako, una ndoto amka nenda kazipambanie ndoto zako mpaka zitimie. Kutimiza ndoto zako sio kama AJIRA/KAZI kwamba ni lazima uwe na uzoefu wa Miaka 5 au 7 ndio uanze kuzifanyia kazi ndoto zako.

Ukiwa na umri wowote ule bado una nafasi ya kutimiza ndoto zako. Bado hujachelewa, anza sasa, anza leo, usiseme utaanza kesho maana moja huna uhakika wa kuiona kesho na pili kitendo cha kuahirisha ni sawa na kuirudisha ndoto yako nyuma kwa muda kadhaa.

Tembelea Ofisi zetu zilizopo SINZA PALESTINA, KARIBU NA GRACE PRIMARY SCHOOL. CALL/SMS/WHATSAPP NOW FOR BOOKING #0659289597