Hanscana: Ataka madirector wachanga wapewe nafasi



Mtayarishaji wa video za muziki nchini, Hanscana amewataka wasanii wa muziki nchini kuanza kuwaamini madirector wachanga ili kuwapa nafasi ya kuonyesha uwezo wao.

Mwongozaji huyo amesema wasanii wengi wamekuwa wakiangalia uzoefu na majina kitu ambacho kinawanyima fursa madirector wachanga wenye vipaji.
“Ufike wakati wasanii muanze kuamini talent, uwezo na sio jina kama ilivyozoeleka na mimi naamini sana uwezo wa madirector wachanga ambao wanaanza,” aliandika Hanscana Instagram.
Aliongeza, “Hivyo basi ifike time nawao pia waaminiwe na wapewe videos kubwa ili kuendelea kusogeza sanaa yetu mbele na iwe ya kiushindani zaidi kama zilivyo South Africa na Nigeria,”
Hanscana ambaye amefanya video nyingi za masta wa muziki ndani ya mwaka 2016, amemtabiria makubwa director mchanga aitwae hopefx.