Roma Mkatoliki ana Mpango wa kufanya Kollabo nje ya Nchi


Roma amemuambia mtangazaji wa Maisha FM ya Dodoma, Silver Touchez “Kufanya collabo na wasanii wa mataifa mengine inakuza muziki wako lakini pia na profile yako inakuwa kwa kuwa unakuwa unatambulika kwenye hiyo nchi nyingine.”
“Ni ngumu kukwambia ninavyopambana kuwa nilikuwa naongea na fulani nataka nipige naye collabo, lakini kila kitu kitakapo kuwa kwenye mstari watashuhudia tu kwa sababu it’s a matter of network na connection tu hakuna uchawi mwingine,” ameongeza.
Katika hatua nyingine msanii huyo amewapongeza rapper wa Bongo ambao tayari wameshafanikiwa kufanya collabo na wasanii wa nje.
Chanzo: Bongo 5