mefahamika kwamba tuzo hiyo mara ya kwanza ilitolewa kimakosa, na mshindi aliyestahili tangu mwanzo alikuwa na King Kiba kutokana na kuwa na wingi wa kura, hivyo sasa ni rasmi Wizkid ameshinda kipengele cha Best Worldwide Act ambacho huamuliwa na majaji wa MTV na Alikiba ameshinda Best African Act kwa mujibu wa kura - katika tuzo hizo zilizofanyika wikiendi iliyopita jijini Rotterdam - Holland.
Taarifa za uhakika kutoka kwenye Management ya Alikiba Exclusive ni kwamba wametumiwa taarifa na MTV EMA kwamba kuna kosa lilitokea lakini wamerekebisha na kumfikishia taarifa Wizkid kwamba tuzo haikuwa yake hivyo itachukuliwa na kupewa Alikiba.
Inaonekana Wizkid amefikiwa na taarifa na tayari post yake ya ushindi wa tuzo hiyo ameifuta kwenye mtandao wake,