Jay Dee atuma Ujumbe huu Baada ya Ruge kusema wapo tayari Kupiga Nyimbo zake

Bosi huyo wa Clouds Media Group, ametoa kauli hiyo Ijumaa ya Wiki iliyopita kwenye mahojiano na kipindi cha XXL cha kituo hicho. “Tatizo ni kwamba hakuna ambacho hatujamaliza, tulimaliza, tunasubiri order. Unajua kimsingi ulipopewa order ya kwamba ‘nyimbo zangu usipige, jina langu usiseme kwenye chombo chako, vyovyote itakavyokuwa mimi sitaki kusikia hiyo kitu’ hiyo ndio order. Kwahiyo labda tukikutana, nimuombe tena @jidejaydee kama tutaruhusiwa kufanya hiyo kitu,” alisema.


Jay Dee


Jide akaandika Ujumbe huu Instagram  Kwahiyo wale mlio omba collabo sijui feat baadae mkaenda kufuta chorus zangu mtafanyaje ??😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Habariiiiiiiiiii zenu buaaaaaana 🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️
#SawaNaWao 

#TofautiNaHesabuZao 

Hii inaonyesha yupo tayari kwa Nyimbo zake kupigwa

Vile vile Siku hiyo Ruge alipohojiwa alisema ana muda mrefu hajawahi kukutana na Lady Jaydee, japo amedai ‘hata leo nikipata nafasi ya kahawa nitashukuru sana kwa huo mwaliko.’