KILIMO KURUPUSHI: KILIMO GANI KINALIPA ZAIDI

Tikiti Maji


Well, sijajua kama ni Ugumu wa Maisha au Kutafuta hela mbadala ndo kunafanya watu wengi tukimbilie shambani, au labda ni Hobby ambayo watu wengi sikuhizi inatujia kwa kasi. Swali la sijajua linakuja pale ambapo mtu anataka kwenda shambani na swali lake la kwanza ni "Nitajie Zao ambalo nikilima nitapata hela nyingi kwa mda mfupi". Hili swali la kwenye Biashara limehamia shambani, ila wanasahau Shambani kuna Risky kubwa zaidi kuliko Biashara za kawaida.

Tushawahi Kulima heka Tatu na tukatoka hola bila hata Mia, na tushawahi kulima heka mbili na tukatoka na Kicheko shambani. Kwakua tunapenda Kulima, tunajua hasara za huku, na tunajua faida za huku. Watu wengj tunafanya Kilimo Kurupushi kutokana na hadithi za "Kilimo kinalipa", na fulani alilima zao fulani akatoboa. Huulizi alilima wakati gani, soko lilikuaje, bei yake ilikuaje, kwanini ilikua hivyo, means aliyotumia kuuza na kadhalika.

Kama kwenye Biashara mtu anaanzaga na Duka dogo zen baadae anakuja fungua duka kubwa, Kwanini wewe mkulima hujawahi kulima hata nusu heka leo unataka kuanza na heka tano au tatu? Mwisho wa siku ukizika Milioni Tatu chini unakuja Kulalamika na kusaga meno. Kama ushawahi Kurisiti form four, hauna Haki ya kumsema mdogo aliyefeli form four mwaka huu, bali una wajibu wa kumfundisha uliyopitia na.nini afanye ili atoboe kama wewe. Na kama haujawah Miliki Pikipiki, Huna haki ya Kuongea mbele ya anayemiliki Baiskeli hata kama ni Mkweche.

By Man Dea.