Vijana zaidi ya 3,000 waliokuwa wameajiriwa na Serikali mwezi Juni mwaka huu, hawana ajira tena.

Serikali kupitia Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro imewafukuza kazi waajiriwa wapya 3000 walioajiriwa mwezi June 2016 na kusainishwa mikataba yote ya kazi. 



Vijana hao waliajiriwa kwa kufuata taratibu zote za utumishi na walipangiwa kufanya kazi kwenye vituo mbalimbali vya kazi ambapo waliripoti na kuanza kufanya kazi, kabla ya kupewa barua za kusitishiwa ajira zao mwezi July kwa kigezo cha uhakiki.

Uhakiki ulipoisha hawakurudishwa kazini, na walipofwatilia walitamkiwa kuwa hawatambuliki. Wanajiuliza kwanini hawatambuliki wakati wana mikataba ya kazi na walishafanya kazi mwezi mmoja kabla ya ajira zao kusitishwa?

Serikali imewataka vijana hao kuwa na subira hadi ajira mpya zitakapotangazwa ili waombe upya. Vijana hao waliajiriwa katika idara na taasisi mbalimbali za serikali kama vile sekta ya Afya, Mahakama, Halmashauri mbalimbali.

Chanzo:JamiiForum