MKWASA: WACHEZAJI WETU NI KAMA HOMA YA VIPINDI

Siku moja baada ya kukamilika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara kocha mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Charles Boniface Mkwasa amesema ni vigumu kupima viwango vya wachezaji hasa wa Tanzania.



Ligi hiyo imemaliza mzunguko wa kwanza huku baadhi ya wachezaji waliong’ara msimu uliopita wakishindwa kufanya hivyo msimu huu huku wachezaji wengine wakiibuka na kung’ara.

Baadhi ya wachezaji waliong’ara raundi ya kwanza ni Shiza Kichuya, Omar Mponda, Simon Msuva wameng’ara raundi ya kwanza na kuzingia timu zao mabao muhimu huku wachezaji kama Nadir Haroub na Abdi Banda wakishindwa kufurukuta na kujikuta wakipoteza nafasi ya kucheza katika timu zao.

Akizungumza na gazeti hili baada ya mchezo wa mwisho wa raundi ya kwanza ya Ligi Kuu kati ya Ruvu Shooting na Yanga Mkwasa alisema tatizo la wachezaji wengi wa Tanzania ni kutokudumu katika viwango vyao hali inayofanya hata kikosi cha timu ya taifa kubadilika mara kwa mara. “Nimeangalia mechi kadhaa za Ligi Kuu, tatizo tulilonalo ni lilelile, wachezaji wetu hawadumu katika viwango vyao.

Unaweza kumwona anafanya vizuri lakini baada ya miezi miwili mitatu akapotea. #mwananchi