Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar limewataka wananchi wanaofanya vitendo vya uhalifu kuacha mara moja.

Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema wanaofanya  vitendo vya uhalifu katika maeneo yao kuacha mara moja kutokana na operesheni  inayotarajiwa kufanyika siku za hivi karibuni ikiwemo katika maeneo ya kigogo jijini Dar es salaam.




Hatua hiyo inakuja  katika ziara ya Mkuu wa Mkoa  Paul Makonda alipokuwa akihitimisha ziara ya siku kumi katika Wilaya ya Kinondoni ambapo  jeshi hilo limewataka wazazi kukanya watoto wao  kwa vitendo wanavyovifanya ikiwemo ni pamoja na  ukabaji wa raia kufuatia  malalamiko yaliyotolewa na wakaazi wa eneo hilo  ambapo wamedai kuwa watoto wa viongozi katika  maeneo hayo wanaojishuhulisha na vitendo vya uhalifu pasipo kuchukuliwa hatua za kisheria.

Aidha Kamanda Sirro amesema kuna baadhi ya watu wanawatambua wahusika wanaofanya matukio ya  uhalifu katika mitaa yao  lakini hushindwa kutoa ushirikianao wa kutosha kwa jeshi hilo jambo ambalo huwakwamisha.